LHRC Yavitaka Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Kuchukua Hatua Dhidi ya Wahalifu...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeviomba vyombo
vya ulinzi na usalama nchini kuwachukulia hatua kali watu wote
wanaoshiriki katika vitendo vya uhalifu.

Ombi hilo limetolewa jijini dar es salaam na mkurugenzi
mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu dkt hellen kijo bisimba wakati
akitoa tamko la maadhimsho ya siku ya amani duniani.
Dkt. Kijo-Bisimba amesema endapo vitendo vya uvunjifu wa
amani vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu nchini vitafumbiwa macho
vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Aidha bi kijo amewataka wananchi kutambua kwamba wao ndio
walinzi wa kwanza wa amani nchini hivyo wanapaswa kufuata sheria na kuepuka
vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
Kila ifikapo septemba 21 dunia huadhimisha siku ya amani
duniani ambapo kwa mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 1981 baada ya
kuidhinishwa na mkutano mkuu wa umoja wa mataifa ikiwa na lengo la kuimarisha
wazo la amani ndani ya baraza la umoja wa mataifa.
Kauli mbiu ya siku amani duniani kwa mwaka 2017 ni “pamoja
kwa ajili ya amani, nidhamu, usalam na heshima kwa wote”
No comments:
Post a Comment