Breaking: JUKATA Waandaa Maandamano Makubwa Nchi Nzima Kudai Katiba Mpya..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
KUFUATIA Serikali ya Rais John Magufuli kuendelea kukaa kimya Juu ya Mwendelezo wa Kukamilisha Mchakato wa Katiba Mpya huku viongozi wa dini na Wanasiasa wakishinikiza juu ya suala hilo.
Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) leo limeibuka na kutangaza maandamano nchi nzima ya amani kwa ajili ya kudai katiba hiyo kwa kutaka serikali kuendeleza mchakato.
Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya ya mkutano Mkuu wa Jukwaa hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho Wa wiki iliyopita wamezimia kifanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya.
"Tumeazimia kufanya maandamano siku ya tarehe 30 ya mwezi huu, katika ngazi ya kitaifa ambayo yatafanyika Jijini Dar es Salaam,yakianzia ofisi za JUKUTA hapa Mwenge Saa nne asabuhi na yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja" amesema Mwakagenda.
Mwakagenda amesema Jukwaa la hilo ni teyari limeshaliandikia barua Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa taarifa juu ya kusudia kufanya maandamano hayo
"Maandamano haya ni ya amani ili kurudisha hamasa ya wananchi kuendelea kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia hapa nchini"
"Kwa upekee na heshima kubwa sana JUKATA pia tumemwandikia barua Rais Magufuli kumwomba ayapokee maandamano yetu ya amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja" Amongeza Kusema Mwakagenda.
Hata hivyo,Mwakagenda amesema kuwa maandamano hayo kwa upande Wa Mikoa mingine nje ya Dar Maandamano ambapo yatafanyika kila wilaya.
Pamoja na hayo JUKATA wamesema wanaamini watapata ushiriano Wa kutosha Wa Jeshi la Polisi ili maandamano hayo yafanyike kwa amani.
No comments:
Post a Comment