Sport News: Je ni Bilionea Mohammed Dewji Kukabidhiwa Simba leo?..Soama Habari Kamili na Matukio360..#share



KLABU ya Simba huenda leo ikaingia kwenye ukurasa mpya wa uendeshaji wa timu ambapo kamati maalum ya kusimamia mchakato wa zabuni ya kumpata mwekezaji kwenye muundo mpya wa klabu ya hiyo kesho Saa 5:00 asubuhi inatarajiwa kukutana na Waandishi.
Bilionea Mohammed Dewji ni mwanachama pekee ambaye ameonyesha hadharani kwa muda mrefu matamanio ya kumiliki hisa asilimia 5i za Klabu hiyo.

Ni dhahiri  wanachama, wapenzi wa klabu ya Simba na wapenda soka nchini wanashauku kubwa ya kutaka kujua nani atakuwa mmiliki mkuu wa klabu hiyo inapoingia katika mfumo mpya wa kujiendesha kibiashara.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu, Haji  Manara imesema kwamba mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Kivukoni 3 uliopo ndani ya hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam.
Kamati hiyo iliyoundwa mapema mwezi uliopita, ipo chini ya Mwenyekitil, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na Wajumbe wengine wanne, ambao ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru, Wakili Dk. Damas Ndumbaro na Yusuph Maggid Nassor.

Agosti 20, mwaka huu wanachama 1,216 wa klabu ya Simba waliridhia mfumo wa klabu yao kuuza Hisa baada ya Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (MNICC), Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Afya Jinsia na Watoto, Dk Hamisi Kigwangala, Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Salim Abdallah 'Try Again' alisema kwamba asilimia 50 ya hisa zitauzwa kwa mwekezaji au wawekezaji watakaoungana wasiozidi watatu, kwa sharti moja tu la kuwa wanachama wa klabu hiyo.  Mwekezaji anatakiwa kuweka dau lisilopungua Sh. Bilioni 20 ili kupatiwa asilimia 50 ya hisa za klabu, wakati kwa kuanzia wanachama wote wa Simba wamepewa asilimia 10 ya hisa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search