Real Madrid yaondolewa kuwania taji La Liga...soma habari kamili na matukio360..#share


Na mashirika ya kimataifa
TIMU ya Real Madrid imepoteza matumaini ya kuwania taji la ubingwa wa La Liga baada ya leo kukubali kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Barcelona.

Sasa Barcelona inaongoza ligi mbele ya Real Madrid iliyonafasi ya nne kwa tofauti ya pointi 14.

Lionel Messi akifanya vitu vyake mbele ya wachezaji wa Real Madrid

Barcelona iliyokuwa ugenini  ilionyesha mchezo mzuri na shambulio la kipindi cha pili cha mchezaji  Luis Suarez na penalti ya Lionel Messi baada ya Dani Carvajal kupewa kadi nyekundu kwa kunawa mpira, bao lililosaidia Barcelona kupanda juu ya jedwali kwa alama 14 dhidi ya Real.

Karim Benzema alipiga mwamba wa goli na kukosa nafasi mbili za wazi katika kipindi cha kwanza , lakini timu hiyo ya nyumbani ilibaki bila jibu katika mechi hiyo ya El Clasico.

Los Blancos ilianza huku Gareth Bale akiwa benchi, na ijapokuwa alimlazimu kipa Marc-Andre ter Stegen kuokoa mipira baada ya kuingizwa kufuatia kutolewa kwa Carvajal, mshambuliaji huyo wa Wales alishindwa kuokoa timu yake.

Badala yake mchezaji wa ziada Aleix Vidal aliongeza chumvi katika kidonda katika dakika za lala salama kwa kupata bao la tatu.


Ni mara ya kwanza  kwa Barcelona  kushinda  mechi tatu za ugenini mfululizo katika uwanja wa Bernabeu, na matokeo hayo yanakiwacha kikosi cha Zinedine Zidane katika nafasi ya nne.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search