Patrobas Katambi aishushia tuhuma nzito Chadema....soma habari kamili na matukio360....#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amedai lengo la kuundwa kwa Ukawa ni Chadema kuviua vyama vingine vya upinzani na lengo hilo limefanikiwa.
Pia amesema wabunge 15 wa Chadema wanatarajia kukihama chama hicho na ameeleza sababu saba zilizofanya kujiondoa katika chama hicho
Pia amesema wabunge 15 wa Chadema wanatarajia kukihama chama hicho na ameeleza sababu saba zilizofanya kujiondoa katika chama hicho
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Patrobas Katambi akitoa sababu za kikihama chama mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, ametaja sababu kuwa ni viongozi kushindwa kukijenga chama kuwa taasisi na kinaendeshwa
kibinafsi.
Nyingine ni ukosefu wa
maamuzi shirikishi, ukiukwaji wa katiba na misingi ya kidemokrasia, ukosefu wa
mawasiliano na umoja, ukosefu wa maadili ya kiuongozi, ufujaji na matumizi
mabaya ya mali za chama na fedha na chama kukosa ajenda za kitaifa.
Katambi amesema ameamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na
upotoshwaji ambao umekuwa ukifanywa na viongozi na wanachama wa Chadema wakidai
kwamba amenunuliwa.
Akizungumzia kuhusu wabunge hao 15, amesema wapo njiani
kukikimbia chama hicho kutokana na kutoridhishwa na namna kinavyoendeshwa na
kwamba kwa sasa wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kulinda maslahi au nafasi
walizonazo ndani ya chama.
Kuhusu Ukawa;
Katambi amesema lengo la kuundwa kwa Ukawa lilikuwa ni
Chadema kuviua vyama vingine vya upinzani ambapo ameeleza kuwa lengo hilo
limefanikiwa.
“Kuundwa kwa Ukawa kulikuwa na makubaliano mawili ya ndani na
nje, kwa nje wapo walioamini kuwa muungano huu utakuwa wa mapigano ya kitaifa,
mfano CUF waliamini hivyo lakini kwa ndani Chadema lengo ilikuwa ni kuviua
vyama vingine,” amesema.
Amesema hadi sasa lengo hilo limekamilika. Akitoa uthibitisho
huo amesema ndiyo maana vyama vingine kama CUF, NCCR-Mageuzi na NLD viko
dhofuli hali huku Chadema kikiwa na nguvu na kwamba kwa sasa Ukawa haupo tena.
Novemba, 2017 Katambi akiwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa
Chadema (Bavicha) mbele ya mkutano wa NEC alitangaza kujivua nyadhifa zote
ndani ya chama cha Chadema na kujiunga na CCM kwa madai kutoridhishwa na
mwenendo wa chama chake.
No comments:
Post a Comment