Madaktari wasimamishwa kwa kumfanyia upasuaji asiyestahili ...soma habari kamili na marukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
Madaktari Hospitali ya Kenyatta nchini Kenya wamesimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.
Taarifa kutoka mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, zinabainisha kuwa wagonjwa wawili waliokuwa hawajitambui na mmoja kati yao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu ilionekana imeviria.
Lakini pia mkurugenzi huyo ameomba radhi na kusema "tunafurahi kuwatangazia umma kwamba mgonjwa huyo sasa ametibiwa na anaenedelea vizuri"
Wafanyakazi wanaochunguzwa katika sakata hilo ni pamoja na daktari wa upusuaji wa ubongo, muuguzi, mtalaam wa dawa za usingizi.
No comments:
Post a Comment