Sababu sita kukamatwa mchungaji KKKT ... soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu
SABABU sita zinadaiwa kuwa ndio chanzo cha mchungaji Fredy Njama wa Usharika wa Karanga, KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Moshi aliyekamatwa na Polisi kwa kinachodaiwa kuwa ni “Uchochezi”.
Mchungaji huyo wiki mbili zilizopita alisoma ripoti katika mkutano mkuu wa mwaka wa usharika wake ambayo ndo imepelekea kukamatwa kwake.
Katika ripoti hiyo, alibainisha kuwa mapato ya usharika yanapungua kwa sababu mbalimbali. Katika utangulizi wa ripoti hiyo alitaja changamoto sita zinazoikabili nchi kwa sasa:
- Ukosefu wa ajira kwa vijana
- Hali ya uchumi inayoyumba
- Hali ya kisiasa ni ya mashaka
- Gharama kubwa za matibabu
- Sera ya elimu bure
- Wastaafu kutolipwa mafao yao.
- Hali ya uchumi inayoyumba
- Hali ya kisiasa ni ya mashaka
- Gharama kubwa za matibabu
- Sera ya elimu bure
- Wastaafu kutolipwa mafao yao.
Ripoti hiyo pia imechapwa ktk kijitabu na kiwanda cha uchapaji cha Dayosisi hiyo.
Kundi la Polisi na maafisa usalama walimchukua Ijumaa asubuhi hadi kiwandani na kumtaka akusanye vijitabu vyote hadi vilivyosambazwa na kuvikabidhi Polisi. Aidha walimtaka aandike barua kuomba radhi na kufuta ripoti hiyo.
Jioni ya juzi, Polisi walifika ofisi ya usharika na kufanya upekuzi. Walichukua laptop na flash. Kisha walimpakia mchungaji katika gari lao na kuondoka naye.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment