Takukuru yamkamata afisa TRA, Mahakama kwa rushwa....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Temeke imewakamata watuhumiwa wawili kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa No. 11,2007 kifungu cha 15.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, watu hao ni maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Kigamboni pamoja na ustawi wa jamii mahakama ya mwanzo Buguruni.

"Mnamo Februari 15, 2018 Bi. Seire Andrea Akilimali, afisa ustawi wa jamii (production Officer) wa mahakama ya mwanzo ya Buguruni alifikishwa mahakama ya wilaya ya Temeke na kufunguliwa kesi Namba 136/18. Hii nikutokana na mtego ulioandaliwa na Takukuru ambapo alikamatwa akiomba rushwa ya sh. 300,000 na kupokea kiasi cha sh. 200,000 ili aweze kumsaidia mwananchi mmoja ( jina limehifadhiwa) ambaye ndugu yake alihukumiwa kutumikia kifungo cha miezi minane ili aweze kupata unafuu wa kutumikia kifungo cha nje,"

Vilevile, Februari 28, 2018 Straton Sylvester Mutayabarwa Afisa wa TRA Kigamboni alifikishwa mahakama ya wilaya Temeke na kufunguliwa kesi Na. 180/18 baada ya kupokea rushwa ya sh.300,000 kutoka kwa mwananchi mmoja (jina limehifadhiwa) ambaye ni mmiliki wa bucha ili asimchukulie hatua za kisheria kwa kosa la kifanya biashara bila kuwa na electrofiscal device (EFD) mashine na kitofuata sheria za kodi.

Taarifa imesema kesi zote mbili zinaendelea kusikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Temeke na watuhumiwa wote wapo nje ya dhamana.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search