Tetesi za soka Ulaya leo Jumamosi....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema mlinzi wa kati Gary Cahill na mshambuliaji Alvaro Morata wanahitaji juhudi zaidi iwapo wanataka kurejea katika kikosi cha kwanza na kuweka uwezekano wa kuziwakilisha timu zao za taifa ambazo ni Uingereza na Hispania.(Express)
Antonio Conte
Real Madrid imekubali kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 pia anafuatiliwa na klabu za Chelsea na Manchester United.(Mundo Deportivo )
Mlinzi wa kati wa Real Madrid Raphael Varane amesema Manchester United inamuhitaji. Mfaransa huyo mwenye miaka 24 alisajiliwa klabuni hapo chini ya Jose Mourinho.(Cadena Ser, via Sun)
Kiungo wa zamani wa Liverpool na Bayern Munich Dietmar Hamann amesema Bayer wanazungumza na kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino juu ya uwezekano wa kuwanoa.(Sky, via Mirror)
Everton wapo tiyari kumlipa kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ambaye mkataba wake na Gunners unaisha mwisho wa msimu huu.Wapo tiyari kumpa paundi milioni 8 kwa mwaka iwapo atasajiliwa bure.(Times )
Borussia Dortmund wameonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Westham mreno Domingos Quina.(Sun)
Spurs wanatarajia kufanya mazungumzo ya kumpa mkataba mpya mshambuliaji raia wa Korea Kusini Son Heung-min.Mkataba wake wa sasa unaishia mwaka 2020.(Sky Sports)
Meneja msaidizi wa Leicester city Michael Appleton yupo miongoni mwa makocha wanaowaniwa na West Brom kuziba nafasi ya Alan Pardew.(Telegraph)
Mlinda mlango wa Roma Alisson anahusishwa kujiunga na Liverpool lakini matamanio yake ni kwenda Real Madrid.(Express)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search