Tshishimbi mchezaji bora Februari....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KIUNGO wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshitshimbi amechaguliwa kuwa
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari, mwaka
huu.
Papy Kabamba Tshitshimbi
Mchazaji huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ametwaa tuzo hiyo akiwashinda mshambuliaji Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi na kiungo mwenzake wa Yanga, Pius Buswita.
Katika mwezi Februari, Okwi aliongoza kwa kufunga mabao,
akifunga mara nne akifuatiwa na Tshishimbi matatu na Buswita mawili.
Lakini Tshishimbi alikuwa na pasi ya bao(assist) pia kwenye mwezi huo
na bahati nzuri kwake hakuonyeshwa kadi yoyote, wakati Okwi alionyeshwa kadi ya
njano.
Kingine kilichombeba Tshishimbi kumbwaga Okwi ni kuiwezesha Yanga SC kukusanya pointi 12 Februari, wakati Simba ilivuna pointi 10 tu.
Kwa ushindi huo, Tshishimbi atazawadiwa fedha taslimu Sh.
Milioni 1 kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja
na kisimbuzi (decoder) kutoka kwa wadhamini wa matangazo wa Ligi hiyo, Azam TV
na ngao ya kumbukumbu ya ushindi wake.
No comments:
Post a Comment