UTAFITI:Upungufu mbegu za kiume unahatarisha maisha.... soma habari kamili na matukio360....#share

Na mashirika ya kimataifa
Wanaume wenye mbegu chache za kiume wako katika hatari ya kupata magonjwa kulingana na utafiti mpya.
Utafiti uliofanyiwa wanaume 5.177 ulibaini kwamba wanaume wenye mbegu chache za kiume wana mafuta mengi mwilini , shinikizo la damu na mafuta machafu katika mishipa ya damu.

Pia wana uwezo mkubwa wa viwango vidogo vya homoni za kiume. Waanzilishi wa utafiti huo wamesema kuwa , wanaume wenye mbegu chache za kiume pia ni muhimu kufanyiwa vipimo vingine vya magonjwa mengine.
Utafiti unatolewa ikiwa ni siku chache serikali  kuthibitisha matumizi ya dawa tano za asili ikiwamo za kuongeza nguvu za kiume
Huku miongoni mwa dawa hizo ni dawa ya 'Ujana' ambayo kazi yake ni kusaidia kuongeza nguvu za kiume wakati dawa nyingine zikiwa Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver ambazo kazi yake ni kukemea vimelea mbalimbali.
Baraza la dawa nchini limesema hatua hii imekuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na kubaini kuwa dawa hizo hazina madhara kwa afya ya binadamu hivyo hawana budi kuzikubali.
Aidha Paul Muhame ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa za asili nchini Tanzania anasema baada ya baraza kupitisha vigezo vyote vilivyohitajika kutoka katika dawa hizo na mamlaka ya dawa na chakula wamethibitisha hilo.
"Suala la muhimu ambalo tumeliangalia zaidi ni usalama wa mtumiaji lakini katika upande wa kuthibitisha kuwa dawa hizo zinaponyesha au la, linabaki kwa mnunuaji na mtumiaji wa dawa hiyo''.
'Hatari'
Upungufu wa mbegu za kiume na matatizo ya ubora wa mbegu hizo ni maswala yanayoathiri mmoja kati ya wanandoa watatu kushika mimba kulingana na utafiti huo uliofanywa nchini Uingereza.
Lakini katika utafiti huu mpya wanasayansi walichanganua wanandoa wasioweza kupata watoto nchini Itali kujua iwapo ubora wa mbegu hizo pia unaathiri afya ya mtu kwa jumla.
Waligundua kwamba wanaume wengi walio na mbegu chache walikuwa na matatizo kadhaa ya kiafya ikiwemo mwili ulionenepa na shinikizo la damu.
Hatua hiyo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo na kiharusi.
Wanaume hao pia walionekana kuwa na viwango vya juu vya kuwa na homoni chache za kiume ambazo hupunguza ukubwa wa misuli na mifupa na huenda vikasababisha ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa.
Daktari Albert Ferlin ambaye aliongoza utafiti huo , alisema: Wanaume wasio na rutuba hukumbwa na matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuhatarisha hali yao ya maisha na kupunguza kiwango cha maisha wanayoishi. ''Rutuba huwapatia wanaume fursa isio ya kawaida ya kutathmini afya na kuzuia magonjwa''.
Hatahivyo wamiliki wa utafiti huo walisisitiza kuwa utafiti wao haukuthibitisha kuwa ukosefu wa mbegu za kiume za kutosha husababisha matatizo ya kimetaboliki lakini badala yake ni vitu viwili vinavyohusiana.
Wanasema kuwa uhaba wa homini za kiume uhusishwa na matatizo haya ya kiafya.
Dr. Ferlin alisema kuwa utafiti unaonyesha kwamba ni muhimu kwamba wanaume wanaotibiwa matatizo ya ukosefu wa rutuba wanafaa kuangaziwa vizuri kimatibabu.
''Wanaume walio na matatizo ya kuwapatia mimba wake zao wanafaa kukaguliwa vizuri na kufuatiliwa na wataalam wao wa rutuba kwa sababu huenda wana viwango vya juu vya kupata maradhi na vifo'', alisema.
Hatahivyo uthibitisho wa dawa hizo nchini Tanzania umezua mjadala mkali katika vipindi vya radio nchini humo haswa katika upande wa serikali kuthibitisha dawa ya nguvu za kiume kuuzwa kihalali .

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search