Vigogo watano TPDC wakabidhi pasipoti mahakamani.... soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu Dar es Salaam.

VIGOGO watano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) wanaokabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya madaraka, wamewasilisha hati zao za kusafiria  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na zimepokelewa.

Hati hizo zimewasilishwa leo mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Emmanuel Jacob.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 18,2018 kwa ajili ya kutajwa.


Washtakiwa wanakabiliwa na kesi hiyo ni  Mkurugenzi Mtendaji, James Mataragio, Kaimu Meneja wa uvumbuzi, George Seni, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na utawala, Wellington Hudson, Mkurugenzi wa Mkondo wa juu,Kelvin Komba na Edwin Riwa ambaye ni kaimu Mkurugenzi wa mipango.



Washtakiwa hao, wanadaiwa kuwa  kati ya Aprili 8,2015 na Juni 3,2016 wakiwa watumishi wa umma na waajiriwa wa TPDC kwa nafasi zao, wakati wakitimiza majukumu yao kwa makusudi walitumia madaka vibaya.

Kwa kubadilisha na kupitisha bajeti na mpango wa mwaka wa manunuzi wa mwaka 2014/2015 na 2015/2016 kwa kuingiza ununuzi wa kifaa cha utafiti cha airborne gravity gradiometer survey ndani ya ziwa Tanganyika  bila ya kupata kibali cha bodi  ya wakurugenzi ya shirika.

Wanadaiwa kuwa kitendo  hicho kinakiuka kifungu cha 49(2) cha sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kwa lengo la kujipatia manufaa yasiyohalali ya dola 3,238,986.50 ambacho ni sawa na Sh 7.2 bilioni kwa Bell Geospace.

Baada ya kusomewa shtaka hilo,washtakiwa wote walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mashauri aliwaachia huru washtakiwa hao baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa  na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh 1 bilioni.

Wadhamini hao walitakiwa kuwa na barua za utambulisho kutoka kwa viongozi wa mtaa, vijiji ama za waajili wao na vitambulisho.

Washtakiwa wasalimishe hati zao za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya jiji la dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Deogratius Lyimo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search