Wambura afungiwa maisha katika soka, apinga uamuzi huo .... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia Michael Wambura kifungo cha kutojihusisha na mpira wa Miguu maisha kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013. Baada ya kupatikana na makosa matatu

Michael Wambura

Hata hivyo Wambura amesema kikao kilichomfungia hakina uhalali hivyo yeye anawajibika kwenye kamati ya utendaji na mkutano mkuu na sasa anasubiri barua kwa hatua nyingine.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa kosa la kwanza alilokabiliwa nalo Wambura ni kupokea fedha za TFF. Pili, malipo yasiyo halali na tatu ni kugushi barua na kushusha hadhi ya TFF.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search