Watu milioni 1.7 nchini hawaoni vizuri.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
TAKRIBANI watu 1,740,000 nchini wanakadiriwa kuwa na tatizo la kutokuona vizuri huku asilimia 70 hadi 90 ya wenye ugonjwa huo hawajijui.
Pia asilimia 4.2 sawa na watu 440,000 wenye umri zaidi ya miaka 40 wanaugonjwa wa shinikizo la macho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi was habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ugonjwa wa shinikizo la macho
Vilevile takribani watu milioni 253 duniani wana matatizo ya kutokuona, kati ya hao milioni 36 hawaoni kabisa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile ametoa takwimu hizo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya wiki ya kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa shinikizo la macho yaliyoanza jana hadi Machi 17/2018 .
Amesema zaidi ya asilimia 75 ya visababishi vya kutokuona vizuri vinaweza kuzuilika au kutibika huku mwaka 2017, watu 13,240 walihudhuria kwenye vituo vya tiba wakiwa na shinikizo la macho.
"Asilimia 2.8 ya watu wote wenye upungufu wa kutokuona vizuri, sawa na watu milioni 7 duniani wanaugonjwa wa shinikizo la jicho, kati ya hao milioni 4.5 hawaoni kabisa, "amesema.
Amesema shinikizo la macho ndiyo chanzo kinachoongoza kwa idadi ya watu wasioona duniani ambako hakirekebishiki.
Naibu waziri huyo amesema ulemavu wa kutokuona unaosababishwa na mtoto wa jicho au upeo mdogo wa macho kuona unatibika.
"Afrika ugonjwa wa shinikizo la jicho unachangia asilimia 15 ya watu wasioona...unaathiri zaidi watu wenye umri wa miaka 40 na zaidi, "amesema.
Amefafanu kwa nchini asilimia 4.2 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 40 wanaugonjwa huo sawa na watu 440,000.
"....ugonjwa huu hauna dalili zozote wakati wa hatua za awali, huambatana na tatizo la kutokuona mbali (myopia) na kuna uwezekano wa hadi asilimia 20 kuwepo kwenye familia, "amesema.
Maadhimisho hayo yataambatana na utoaji elimu ya Afya ya macho, upimaji wa macho kwenye hospitali nchini.

No comments:
Post a Comment