Ajali yaua Mwanajeshi JWTZ na mtoto...soma habari kamili na matukio360...#share

MWANAJEHI mmoja wa JWTZ pamoja na mtoto wa Mwanajeshi mwenzake wanadaiwa kupoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari la Polisi aina ya Basi lililogongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi wa JWTZ, maeneo ya Bwawani Morogoro

Inadaiwa basi hilo la Polisi lilikuwa likitokea Dodoma huku Noah hiyo iliyokuwa imebeba Wanajeshi takribani 6 pamoja na mtoto wa Wanajeshi mwezao ilikuwa ikitokea Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ingawa amekiri kutokuwa na taarifa za undani zaidi kwa sasa 




Advertisement

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search