Diamond aachiwa kwa dhamana...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz jana alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia kusambaza picha zisizo na maadili.
Mambosasa amesema kuwa Diamond alihojiwa na kupewa dhamana jana Jumatatu huku uchunguzi zaidi ukiwa unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi.
“Alihojiwa jana na akapewa dhamana, upelelezi unaendelea,” amesema Mambosasa.
Leo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema polisi inamshikilia msanii huyo na Nandy ambao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kusambaza picha sisizo na maadili kwenye mtandao.
Wasanii hao wanadaiwa kusambaza picha hizo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.
No comments:
Post a Comment