Lema akamatwa na Jeshi la Polisi...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MBUNGE wa Arusha Mjini  Godbless Lema leo April 27, 2018 amekamatwa na polisi na kufunguliwa kesi mpya kuhusu uchochezi kwa ndoto aliyowahi kuota kuhusu Rais Dk. John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita.

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa Lema leo alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka miwili iliyopita.

"Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa "uchochezi". Dhidi ya Mh Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota. Lema alihudhuria Mahakamani siku ya leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa...Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale" alisema John Mrema

Kesi hii ni mwendelezo wa kesi iliyokua ikimkabili Mh Godbless Lema na ambayo ilimsotesha Mahabusu (Magereza) kwa zaidi ya miezi 4 mwaka juzi kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwaka jana.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search