Mkuchika atoa onyo kwa watumishi wa serikali...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa atawachukulia hatua watumishi wa serikali ambao wanazuia barua za watumishi wengine hasa walimu wanaotaka uhamisho zisimfikie yeye au Katibu au Waziri Mkuu.
George Mkuchika

Mkuchika amesema hayo bungeni na kudai kuwa yapo malalamiko ya baadhi ya walimu kushindwa kuhama kutokana na viongozi wao kuzuia barua zao zisifike kwake au viongozi wengine ambao wana mamlaka.

"Sasa naomba kulieleza bunge hili tukufu mwenye mamlaka ya kumkatalia uhamisho ni yule anaye andikiwa barua

"Wewe uliyeandikiwa pale kupitia kwa kiswahili sanifu kabisa, wakishasema kupitia kwa wewe si muamuzi wa mwisho, peleka barua kwa mwajiri ili mwajiri apate kuamua

"Mimi natembelea mikoani nimepata kupita mkoa mmoja naambiwa hii ofisi yetu haijapitishwa barua ya mtu kuhama hata moja, mimi nasema mimi ndiyo Waziri wa Utumishi wa Umma, nikimbaini kuna kiongozi wa utumishi anakataa kupitisha barua isinifikie mimi, isimfikie Katibu Mkuu Kilimo, isimfikie Waziri Mkuu nitamshughulikia mwa mujibu wa sheria na taratibu 

"Nitafanya hivyo kwa sababu mtu huyo amejichukulia madaraka ambayo si yake,  hukuandikiwa wewe barua halafu wewe ndiye unaamua sasa mimi niliyejuu nitafanya kazi gani kama wewe unaniamulia" alihoji Mkuchika

Mbali na hilo Mkuchika amesema kuwa zoezi la kuajiri sasa linatarajiwa kuendelea baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki kukaribia kukamilika na kusema serikali itaendelea na kutoa ajira mpya.

"Tutaendelea na ajira mpya kama nilivyosema 50,200 wa mwaka jana na mwaka ujao serikali imejipanga kuajiri 49,000" alisema Mkuchika

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search