Polisi waua majambazi wanne...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Pwani
POLISI Mkoani Pwani wameua majambazi wanne asubuhi ya leo walipokuwa wakijaribu kupora maeneo ya Kisarawe mkoani humo.
Kabla ya kuuawa yalitokea majibizano ya risasi kati yao na askari Polisi.
Imedaiwa majambazi hao wametokea jijini Dar es Salaam na walikuwa wanatumia gari lenye namba za kibalozi hatua iliyosababisha askari wa usalama barabarani kutowahisi chochote kwani gari hizo sio rahisi kusimamishwa ovyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani, Evarist Ndikilo amethibitisha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment