TANZIA: Masogange afariki...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

VIDEO queen marufu nchini Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia jioni ya leo jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa katika hospital ya Mama Ngoma akipatiwa matibabu

Akithibitisha taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.

Tayari mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.

Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.


Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni  na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search