Watu 7 mbaroni kwa kuhamasisha maandamano...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WATU saba akiwamo mwanamke mmoja wanashikiliwa na Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amewaambia wanahabari leo Aprili 25 kuwa watu hao wamekamatwa kutokana na sababu za kuhamasisha maandamano Aprili 26 mwaka huu.

Ilembo amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakihamasishana kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwamo ya Telegram na WhatsApp.

Amesema watu hao wamekamatwa kupitia vitengo vya intelijensia baada ya kuwekewa mitego mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata.

Amesema miongoni mwa watuhumiwa hao baadhi yao wapo vyuo vikuu, mitaani na maeneo mengine.

Ilembo ameongeza kuwa watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote, huku wakiendelea kuwatafuta wengine kwa njia mbalimbali.

"Nasisitiza hakuna maandamano Aprili 26, atakayeandamana atavuna alichopanda kwa kuwa Serikali haijaribiwi," amesema Ilembo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search