BENKI YA TPB YAWATOA HOFU WATEJA WOTE WALIOKUWA BENKI YA TWIGA BANCORP...SOMA HABARI KAMILI NA MATUKIO360...#SHARE
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
OFISA
Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi amewatoa hofu wateja wote
waliokuwa kwenye benki ya Twiga Bancorp huku akiwahakikishia kuwa wapo katika
mikono salama na wataendelea kupata huduma kama hapo awali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi
akizungumza na wafanyakazi waliokuwa Twiga Bancorp pamoja na wateja wa benki
hiyo jijini Dar es Salaam wakati anawakaribisha rasmi kutokana na Benki Kuu ya
Tanzania(BoT),kuziunganisha benki hizo.
Moshingi
ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya benki ya TPB kuandaa hafla
fupi ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuwakaribisha wateja na wafanyakazi
waliokuwa kwenye benki ya Twiga Bancorp.
Kwa
kukumbusha tu benki ya TPB na Twiga Bancorp zimeunganishwa Mei 17 mwaka huu baada
ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kutoa tamko rasmi.
"Hakuna
kilichobadilika, huduma zitabaki pale pale, wateja wote mtaendelea kuhudumiwa
katika matawi ya iliyokuwa benki ya Twiga Bancorp mpaka kipindi cha mpito
kikimalizika.
"Kipindi
cha mpito tulichopewa na BoT ni miezi mitatu, ambayo itatupa nafasi kuweka
mitandao ya benki hizi pamoja na kurahisisha katika kutoa huduma za
kibenki,"amesema Moshingi.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Windhoek
Tanzania Simon Salatiel ambaye ni moja ya wateja wa iliyokuwa benki ya Twiga
Bancorp akitoa shukrani zake jijini Dar es Salaam baada ya benki hiyo
kuunganishwa na benki ya TPB Plc.
Kwa
upande wake aliyekuwa Meneja Msimamizi wa iliyokuwa Benki ya Twiga Bancorp,
Nkanwa Magina kutoka Benki Kuu ya Tanzania, amewataka wateja waliokuwa Benki ya
Twiga Bancorp kutokuwa na wasiwasi, kwa kuwa kuunganishwa kwa benki hizo mbili
kumeongeza nguvu katika utendaji wa kutoa huduma za kibenki.
Pia
amesema wafanyakazi waliokuwa katika benki ya Twiga Bancorp, waendelee na moyo
ule ule waliotoka nao kwenye benki yao na kuonesha ushirikiano wa dhati wa
wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya TPB.
Wafanyakazi wa Benki ya TPB Plc(kulia),
wakibadilishana mawasiliano baada ya benki hiyo kuwakaribisha rasmi waliokuwa
wafanyakazi wa benki ya Twiga Bancorp ambapo kwa sasa zimeunganishwa.
Wakati
huo huo waliokuwa wateja wa benki ya Twiga Bancorp, wametoa shukrani zao kwa
uamuzi uliofanywa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuunganisha benki hizo mbili,
kwani ni faraja kwao na kusisitiza watapata huduma kwa ufanisi zaidi.
"Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Serikali ya
Awamu ya tano kwa uamuzi huu waliouchukuwa wakuunganisha benki hizi mbili kwani
umetuondolea wasiwasi sisi tuliokuwa wateja wa Twiga Bancorp,"amesema
mteja aliyefahamika kwa jina la Janet Mmari.
Moja
ya wateja wakubwa wa Benki ya Twiga Bancorp (kulia) akisalimiana na baadhi ya
wafanyakazi wa Benki ya TPB Plc jijini Dar es Saalaam baada ya kufanyika hafla
iliyoandaliwa na benki ya TPB kuwakarabisha wateja na wafanyakazi wa Twiga
kutokana na uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)kuziunganisha benki
hizo.Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi.
No comments:
Post a Comment