Ushahidi kesi Ofisa TRA kusikilizwa kwa siku mbili...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

USHAHIDI  dhidi ya kesi inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa (TRA), Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh.milioni 197.6 yasiyolingana na kipato chake unatarajia kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo.

Hayo yameelezwa leo Mei 2 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Inspekta Hamis kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo, Inspekta Hamis amedai kuwa hana taarifa za kutosha kuhusu usikilizwaji wa shauri hilo kwani lipo chini ya Mawakili wa Takukuru na hawapo mahakamani.Kutokana na taarifa hiyo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 28 na 29, 2018, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa anadaiwa kati ya Machi 21, 2016 na Juni 30, mwaka 2016 maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mfanyakazi wa TRA  alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.Inadaiwa pia, alikutwa akimiliki magari 19, yakiwemo Toyota Ra4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry, Toyota Ipsum na mengineyo ambayo yote yote yana thamani ya milioni.197,601,207

Pia anadaiwa, kati ya Machi 21, 2012 na Machi 30, 2016 maeneo ya Dar es salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu (kifahari) yenye thamani ya Sh.milioni 333.2 tofauti na kipato chake

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search