BIMA YA MAZAO: MKOMBOZI MPYA WA WAKULIMA TANZNIA.
PATA KUFAHAMU UWEPO WA FAIDA KUBWA KWA WAKULIMA ITOKANAYO NA BIMA YA MAZAO YA BIMA
YA MAZAO KWA WAKULIMA!!
Mtandao
wa Vikundi Vya Wakulima Tanzania (Mviwata) , umewataka wakulima nchini kujiunga
na bima ya mazao ili kujikinga na majanga mbalimbali ikikwemo mabadiliko ya
tabia nchi ambayo namechangia ukame na mafuriko hapa nchini.
Mwenyekiti wa
Mviwata ngazi ya Taifa, Veronica Sophu, alisema hayo wakati wa kufunga Mradi wa
majaribio unaoshughulikia changamaoto za wakulima ujulikananao kama
FARMAF.
Mradi huyo wa
FARMAF umefanya kazi katika mikoa mitatu kupitia vikundi vya wakulima.
“Bima ya
mazao, itamsaidia mkulima pale atakapo pata majanga mbalimbali yakiwemo
yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi, mafuriko na ukame, hivyo nawashauri
wakulima wajiunge na bima hii kwa sababu ni mkombozi pale kunapotokea majanga”
alisema
Sophu alisema
hapa nchini, mradi huo ulioanza mwaka 2014 na kukamilika Desemba mwaka
2016 na ulifadhiliwa na Jumuia ya Ulaya na ulijikita katika maeneo matatu
ambayo ni Stakabadhi ghalani, bima ya mazao na mfumo wa masoko unaotumika.
“Mradi huu, hapa
nchini umetekelezwa katika wilaya tatu za mikoa mitatu ambazo ni Mtwara(Masasi
), Manyara(Kiteto) na Dodoma kupitia wilaya ya Kongwa na umekuwa na mafanikio
makubwa kwa wakulim”alisema Sophu.
Kwa upande
wake, Apolo Chamwela ambaye ni mkulima wa Mahindi kutoka
kijiji cha Magumu wilaya ya Kiteto alisema kupitia bima ya mazao ambayo
wameikata katika msimu wa mwaka huu, wanaamini itawasaidia kwa sababu kiasi cha
fedha wanachowekeza katika mashamba hakitapotea kutokana na majanga mbalimbali
yanayotokea ikiwemo ukame na mafuriko.
“ Kupitia mradi huu wa bima ya mazao,wakulima zaidi ya 44 kutoka kijiji cha Magumu kilichopo wilaya ya Kiteto ambapo mradi huu wa majaribio unatekelezwa , tayari wamejiunga na bima”alisema Chamwela.
“ Kupitia mradi huu wa bima ya mazao,wakulima zaidi ya 44 kutoka kijiji cha Magumu kilichopo wilaya ya Kiteto ambapo mradi huu wa majaribio unatekelezwa , tayari wamejiunga na bima”alisema Chamwela.
“Bima hii ni
asilimia nane ya gharama ya mkulima anazotumia katika kilimo na kwamba mtu
anakata bima kulingana na gharama za uzalishaji kwa wale wakulima ambao
wanalima kisasa, heka moja ina gharimu Sh 307000, kwa maana hiyo mkulima
atakata bima ya Sh 24560 kulinda gharama ya hiyo heka moja”aliongeza Chamwela
Naye,
Mratibu wa Mradi huo wa Farmaf kutoka Chuo Kikuu cha Greenwich nchini
Uingereza, Dk Gideon Onumah alisema katika bara la Afrika mradi huo
umetekekezwa katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Zambia na Bukinafaso.
”Nchi ya Zambia,
wakulima wake wao walikata bima kwenye mikopo ya kilimo inayoendana na pembejeo
lakini kwa wakulima wa Tanzania wao wamekatia bima mazao ambayo tayari
wamezalisha na faida ya kukatia bima mazao ni kuwa na usalama wa mazao yao
mpaka pale utakapoenda sokoni kuuza na pia kama mkulima angepata janga
angefidiwa kupitia bima aliyokatwa”alisema Dk Onumah.
Makala
hii imeandikwa na Mwandishi maalum!
No comments:
Post a Comment