Kutoka Kwa Waziri Ummy Mwalimu: Homa ya Ini ni hatari mara 10 zaidi ya 'gonjwa hatari la Ukimwi..' #share

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kati ya 100 watu 8 wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa wa Homa ya Ini bila kuonesha dalili.

Halikadhalika takwimu za awali zinaonesha maambukizi ya ugonjwa huo wa homa ya Ini ni makubwa mara 10 kuliko ugonjwa wa Ukimwi.


Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wakiadhimisha siku ya Homa ya Ini inayofanya na Mataifa mengine Duniani amesema Waziri Ummy,ugonjwa wa Homa ya Ini husababishwa na virusi ambavyo vinavyoingia mwilini mwa binadamu hushambulia ini hali inayosababisha mwathirika wa ugonjwa kupata saratani ya ini.

"Pamoja na virusi hivi pia homa ya ini inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa kiholela,vilevi kupita kiasi,aina mbalimbali za sumu na magonjwa mengine yanayoshambulia kinga za mwili na ini,"alisema Ummy.

Amesema Ummy,takwimu za Shirika la Afya Duniani limeonesha kuwa,vifo vinavyotokana na Homa ya Ini zinaendelea kuongezeka na mnamo wa mwaka 2015 kulikuwa na vifo Milioni 1.34.

Alielieleza kuwa matibabu ya ugonjwa wa Homa ya Ini ni gharama kubwa na ndio maana kinga ni bora kuliko,tiba kwa wagonjwa waliopata kirusi aina ya A na E mara nyingi hutolewa kutokana na dalili za mgonjwa zinazoambatana na ugonjwa huo.

"Ugonjwa wa homa ya ini unaweza kukingwa kwa kutumia chanjo ambayo hutolewa kwa mtu asiye na maanbukizi ya virusi hivyo na maambukizi ya virusi B hutolewa chanjo mtu asiyekuwa na maambukizi ya virusi hivyo hutoa kinga ya maisha.

Aidha aliwataka wajiriwa kuwakinga watumishi wao sehemu za kazi huku Wizara ikiangalia namna gani ya kufikia jamii iliyobaki ili kuweza kuwapatia chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B.

Amesema Wizara ipo katika hatua za kudhibiti Homa ya Ini kwa kuunda kikosi kazi cha Taifa kinachojishuhulisha na wataalamu kutoka taaasisi mbalimbali hivyo pia imeandaa vielelezo vinavyohusu ugonjwa wa homa ya ini ili kuweza kuelimisha umma juu ya ugonjwa huo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi hakuna ushaidi wa ugonjwa wa mlipuko wa ugonjwa huo nchini,wananchi wa Afrika Mashariki na Tanzania wapo katika ya hatari kupata maambukizo ya ugonjwa huo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search