EXCLUSIVE STORY!! NAPE ANENA 'SIHAMI NG'O!!
ASEMA MABADILIKO NDANI KWA NDANI, CHAMA I
Akizungumza na Waziri Mwakyembe na watendaji wengine mjini Dodoma wakati akikabidhi Ofisi kwa Waziri mpya, Nape amesema, "Kwanza sina kinyongo na Rais na ningeomba watu wasinilishe maneno wala kufanya assumption zao. I am stronger than they think, nimelelewa humu ndani na ninazijua ups and downs."
"CCM ni chama Bora sana sana siwezi kutoka. Kwa sasa wanaowaza kuwa labda nitatoka wanapoteza muda. I fought for this party and hata kama yapo mambo ya kurekebisha siwezi kurekebisha nikiwa nje nitarekebisha nikiwa ndani. Kwahiyo I wish walielewe hilo ili tusipotezeane muda", alisema Nape.
"Pia nichukue nafasi hii kumshukuru Rais kwa muda niliofanya nae kazi kwa miezi 15."
"Dkt. Wizara nzuri sana hii, inagusa watu wote bila kujali profession zao. Changamoto kubwa ni sheria zilizopitwa na wakati. Tulijikita kuzibadilisha ziendane na wakati. Tulianza na Habari na tulikuwa tunaelekea kwenye michezo, sanaa n.k. Nadhani wewe Mwanasheria ukiliweza hili uatakuwa umesaidia wizara na nchi pia ili hata mtu mwingine akija baadaye akute misingi ya kisheria ya kufanya mambo"
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akabidhiwa ofisi na Waziri aliyepita Nape Nnauye mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment