Picha 7: Ona Kivuko 'Bomba cha MV kazi' kikiwa 'mzigoni' kwa majaribio ya mwisho mwisho !

Hivi karibuni Blog yako ya Matukio ilikudokeza ujio wa kivuko cha 'Mv Kazi' kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wananchi wa Dar es Salaam, hususan wakazi wa Kigamboni na viunga vyake, leo hii kwa hisani kubwa ya Temesa na blog yako ya jamii tunakuletea picha 7 za kivuko hicho 'muruwa kabisa' kikiwa kwenye anga zake kwa majaribio ya mwisho mwisho !  
... endelea kusoma...










Kivuko cha MV KAZI hatimaye kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari  kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.

Awali wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza  kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo. Zoezi hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.
Miongoni mwa waliokuwepo kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.
Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la Magogoni/Kigamboni.
Source: PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA) 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search