KWA NINI NIMEMTUMBUA MAALIM?? LIPUMBA AFUNGUKA!!


Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) leo limemvua, Maalim Seif nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chama hicho na nafasi hiyo kukaimiwa Bi. Magdalena Hamis Sakaya.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa CUF Taifa, anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa Baraza hilo limefiki uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali ambapo moja wapo ni Maalim Seif kutofika ofisini na kutohudhuria kwenye vikao vya chama vinavyotambulia kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

“Miongoni mwa ajenda tulizo zijadili ni kuthibitisha wakurugenzi na manaibu wakurugenzi, kupitisha jina la wagombea Ubunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kujaza nafasi za wajumbe wa Baraza Kuu zilizokuwa wazi, kuunda Bodi ya wadhamini, kuunda kamati ya maadili, taarifa ya fedha, taarifa ya kesi na taarifa ya hali ya kisiasa,”.

Pia Prof. Lipumba ametangaza majina matatu ya Wagombea Ubunge Bunge la Afrika Mashariki kupitia majina yaliyoteuliwa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichokaa Machi 25 na 26 mwaka huu.

Majina matatu yaliyoteuliwa na Baraza kuu la uongozi la Uongozi ni, Sonia Magogo, Mohammed Habib Mnyaa na Thomas Malima mmoja kati yao akitoa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mbali na hayo, Lipumba amemtangaza rasmi Bw. Abdul Kambaya kuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma ambapo hapo awali alikuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search