Kwa wanaume, kujamiiana hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya tezi dume. Ripoti iliyowasilishwa na American Urological Association ilibaini kuwa wanaume wanaojamiiana mara nyingi huwa na furaha na pia kwa asilimia 20 hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hii ni kwa sababu kutoa manii mara kwa mara huondoa sumu katika korodani.
Vilevile ufanyaji wa mapenzi mara nyingi hupunguza uwezekano wa kuugua mafua na kuondoa bakteria ndani ya mwili.
Watafiti wa chuo cha Wilkes-Barre nchini Pennsylvania wamegundua kuwa, watu wanaojamiiana mara moja au mbili kwa wiki wanaburudika kwa kiwango cha asilimia 30 na pia huimarisha mfumo wa kinga ya mwili (Immunoglobulin A) ukilinganisha na wale ambao hufanya mara chache au wasiofanya kabisa.
‘Immunoglobulin A (IgA)’ ni mfumo unaoulinda mwili dhidi ya virusi na bakteria wa aina mbalimbali.
Madhara ya kupata UTI hupungua kwa kiwango cha kufikia asilimia 80 ndani ya saa 24 mtu anapojamiiana. Wakati wa kujamiiana bakteria ndani ya uke husukumwa kwenye mirija ya mkojo na hutolewa nje. Hivyo kwa wanawake pale wanapoacha kujamiiana huongeza hatari ya kupata maumivu wakati wa kukojoa.
Malumbano ndani ya mahusiano huweza kuanzishwa na; Kutokujamiiana kitu ambacho huichukua furaha, ukaribu na maelewano ndani ya mahusiano.
“Kutokujamiiana ndani ya ndoa kunaweza kupunguza kujiamini na kujithamini na pia hupunguza kiwango cha homoni ambayo hutumiwa na mwili kama dawa na pia kuwezesha kujifungua.” Anasema Les Parrott, ambae ni mwanasaikolojia na mwandishi wa kitabu cha “Saving Your Marriage Before it starts”
Kutokujamiiana kwa muda mrefu huongeza woga na kuhisi kuwa mwenza wako anaweza kuchepuka na kutafuta mwingine ambae atamtimizia haja yake ya kujamiiana kitu ambacho kinaweza kuleta mafarakano ndani ya ndoa.
Lengo la Parrott siyo kwamba wachumba wasiojamiiana hawana furaha, la hasha “kujamiiana ni njia mojawapo ya kuelezea ama kuonesha urafiki uliopo kati ya wenza hao”
Busu, kushikana mikono, na kupeana zawadi husaidia pia kuwaunganisha wapenzi kihisia hata kama wasipokutana kimwili.
Vilevile wanaume ambao hawajamiiani mara kwa mara na wasiojamiiana kabisa huongeza uwezekano wa kupata madhara ya uume kushindwa kusimama. Hii ni kulingana na utafiti uliotolewa na American Journal of Medicine.

Imekusanywa kutoka mitandao mbali-mbali..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search