MATUKIO PICHANI: TANZANIA, ETHIOPIA ZAKUBALIANA KUENDELEZA USHIRIKIANO WA NCHI HIZI MBILI.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh Gabeyehu wakisaini mkataba unaolenga ushirikiano katika kupambana na uhamiaji haramu, masuala ya biashara na mapambano na ugonjwa wa malaria Ikulu Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakisaini mkataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakibadilishana mikataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya utiliaji saini mikataba ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia ambao amemuahidi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali za maendeleo, Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikulu leo Jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia  Mhe. Hailemariam Dessalegn ikulu leo Jijini Dar es Salaam
 PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search