NEWS UPTADES!! RAIS MAGUFULI AUNDA KAMATI 'MCHANGA WA DHAHABU'

JUST IN: RAIS DKT. MAGUFULI ATEUA KAMATI YA UCHUNGUZI WA SHEHENA YA MCHANGA WA KUTOKA MIGODINI

===============================================

Kamati aliyoiteua Rais Magufuli leo March 29 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, leo March 29 2017 ameteua kamati ya wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 8, inatakiwa kuanza kazi haraka iwezekanavyo.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni;
⦁ Prof. Abdulrahman Hamis Mruma
⦁ Prof. Justianian Rwezaura Ikingula
⦁ Prof. Joseph Bushweshaiga
⦁ Dkt. Yusuf Ngenya
⦁ Dkt. Joseph Yoweza Philip
⦁ Dkt. Ambrose Itika
⦁ Mohamed Zengo Makongoro
⦁ Hery Issa Gombela
Wajumbe wote wa kamati hii wanatakiwa kufika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 31 Machi, 2017 saa 4:00 asubuhi.

Source Millard Ayo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search