CCM YATAJA WAGOMBEA WAKE 'EALA'

· 12
KUOMBA RIDHAA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI KUPITIA CCM
·
TUMEZINGATIA
'GENDER' NA UWIANO WA MUUNGANO
![]() |
Majina ya walioteuliwa kugombea. |
Majina yaliyotajwa yamezingatia uwakilishi wa pande zote za muungano, uwiano wa wanawake na wanaume pamoja na uadilifu wa wanachama wenyewe.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama chake kina nafasi sita za uwakilishi lakini wameamua kutoa watu 12 ili kuwapa nafasi kubwa Wabunge kuchagua wanaofaa zaidi.
Walioteuliwa na CCM kutoka bara upande wa wanawake ni Zainabu Kawawa, Happiness Lugiko, Francy Nkuhi na Happiness Mgalula.
Wanaume kutoka bara ni Dk Ngwaru Maghembe, Adam Kimbisa, Anamringi Macha na Charles Makongoro Nyerere.
Kwa upande wa Zanzibar wanawake ni Maryam Ussi Yahya na Rabia Abdallah Hamid. Wanaume ni Abdallah Hasnu Makame na Mohammed Yussuf Nuh.
No comments:
Post a Comment