TRUMPH AMWEKA BINTIYE KUWA MSAIDIZI WAKE IKULU ! NI IVANKA TRUMP

Ivanka Trump (pili kulia) amesema alikuwa akifanya kazi kwa kujitolea;
Cheo chake halisi kitakuwa Msaidizi wa Rais.





age Ivanka Trump amejiunga rasmi na serikali ya babake ambapo atahudumu kama mfanyakazi asiyelipwa, kwa mujibu wa ikulu ya White Hous
Binti huyo wa rais wa Marekani amekubali shinikizo baada ya wataalamu kuhusu maadili kukosoa mpango wake wa awali wa kutaka kuhudumu katika wadhifa usio rasmi.
Bi Trump, 35, amesema amesikia "maswali ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza kuhusu hatua yangu kumshauri rais katika nafasi yangu kama mtu binafsi".
Mumewe, Jared Kushner, ni mshauri mwandamizi wa Rais Donald Trump.
Kupitia taarifa, White House imesema ina furaha kwamba "Ivanka Trump amechukua hatua hii isiyotarajiwa katika nafasi yake kama binti wa rais".




Justin Trudeau na Ivanka Trump White House 13 Februari 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIvanka Trump amekuwa akihudhuria mikutano ya Trump na viongozi wa dunia

Bi Trump alisema kupitia taarifa yake kwamba amekuwa akifanya kazi "kwa nia jema na kundi la washauri wa rais White House pamoja na mshauri wake binafsi kujadili kuhusu jukumu lake".
Wataalamu kuhusu maadili walilalamika ilipobainika wiki iliyopita kwamba Bi Trump angepewa afisi White House pamoja na kibali cha usalama cha kuingia na kuondoka ikulu hiyo, bila yeye kujiunga rasmi na wahudumu wa rais.
Wakosoaji walisema kazi ya Bi Trump inafaa kufanywa rasmi ndipo aweze kudhibitiwa na sheria kuhusu uwazi wa maafisa wa serikali pamoja na maadili. Aidha, adhibitiwe na sheria kuhusu mgongano wa maslahi.
Wakili wa Bi Trump, Jamie Gorelick, amesema mteja wake atawasilisha nyaraka zifaazo za kufichua utajiri wake kwa mujibu wa sheria kuhusu maadili ya watumishi wa umma Marekani.




Ivanka Trump naAngela Merkel. : 17 Machi 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWiki mbili zilizopita, Bi Trump aliketi pamoja na Angela Merkel, kiongozi huyo wa Ujerumani alipokuwa ziarani Marekani
Source: BBC Swahili

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search