WABUNGE WA CCM WALIOPANGA KUMUONA LEMA GEREZANI WAONYWA, WAITWA WASALITI

Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni. 

Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.

Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.

Rais amewaambia wabunge wa CCM kuwa yeye ndio aliyekataza bunge lisionakene "live" (mubashara)



CHANZOGazeti la Mwananchi.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search