CHIBU PERFUME YA DIAMONDPLUTNAMZ YAZINDULIWA RASMI.. KUPATIKANA MADUKA YOTE YA GSM

9
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akiwasili kwenye maduka makubwa ya GSM Mall Barabara ya Nyerere leo tayari kwa kuzindua Pafyum yake inayoitwa (CHIBU), Diamond akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo amesema ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza pafyum zenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini.
Ameongeza kwamba kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
11
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa Mameneja wake Babu Tale.
12
Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo.
13
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni.
1415
Meneja wa Diamond Plutnamz Bw. Salaam Medes akizungumza mara baada ya kuzindua pafyum hiyo kwenye duka kubwa la GSM Mall barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo.
16
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha chupa ya pafyum ya CHIBU aliyoizindua leo jijini Dar es salaam.
17
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akimkabidhi chupa ya Pafyum Aisha Azori mteja wake wa kwanza aliyenunua bidhaa hiyo kwenye maduka ya GSM Mall jijini Dae salaam.
18
Bw. Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo jijini Dar es salaam.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search