DSE: Mauzo soka la hisa yapungua...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed
Na Salha Mohamed, Dar es salaam
THAMANI ya mauzo ya soko la hisa (DSE), imepungua kutoka bilioni 4 Novemba 30, 2017 hadi bilioni 3.7 Desemba 8, 2017.
THAMANI ya mauzo ya soko la hisa (DSE), imepungua kutoka bilioni 4 Novemba 30, 2017 hadi bilioni 3.7 Desemba 8, 2017.
Mary Kinabo
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mwandamizi wa
Masoko, Mary Kinabo amesema mbali na kupungua kwa mauzo, idadi ya hisa
zilizouzwa na kununuliwa imepanda.
"Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka
hisa milioni 7.6 ya wiki iliyoisha Novemba 30/2017 hadi hisa milioni 8 ya
wiki inayoishia Desemba 8/2017",amesema.
Amesema ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika
soko umepungua kwa shilingi bilioni 433 kutoka shilingi trilioni 21 wiki
iliyopita hadi shilingi trilioni 20.8 wiki iliyoishia Desemba 8/2017.
Amefafanua kuwa punguzo hilo ni kutokana a kushuka kwa bei za
Uchumi Supermarket Ltd(USL) kwa asilimia 10,Acacia Mining (ACA) kwa
asilimia 10,Kenya Commercial Bank(KCB) kwa asilimia 5 na DCB kwa asilimia 1.
Amesema ukubwa wa mtaji katika Kampuni za ndani umepanda kwa
shilingi bilioni 88 kutoka trilioni 10.035 hadi kufikia shilingi trilioni 10.13
wiki hii kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za kampuni ya bia TBA kwa asilimia
2.
Amesema kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko
(DSEI) kimepungua kwa point 45 kutoka point 2,207 hadi point 2,162
kutokana na kushuka kwa bei ya hisa za Uchumi Supermarket Ltd (USL), Acacia
Mining (ACA), Kenya Commercial Bank (KCB).
"Kiashiria cha sekta ya Viwanda kimepanda kwa point 78
kutoka pointi 5,293 hadi pointi 5,372,"amesema.
Amesema mauzo ya hati fungani katika wiki inayoishia Desemba
8/2017 yalikuwa shilingi bilioni 1.4 kutoka shilingi milioni 17 wiki iliyopita
Novemba 30/2017.
"Mauzo haya yalitokana na hatifungani 5 za serikali zenye
jumla ya thamani ya shilingi bilioni 1.6 kwa jumla ya gharama ya shilingi
bilioni 4,"amesema.
No comments:
Post a Comment