HABARI NA MATUKIO PICHANI: ABBAS AIPONGEZA BOT KWA KUELIMISHA WAANDISHI WA HABARI

MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kwa kuandaa semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, iliyomalizika mjini Unguja, Zanzibar leo Machi 31, 2017.
Dkt. Abaasi alisema, BoT, kama taasisi ya serikali inao wajibu wa kuwapatia habari wananchi kupitia waandishi wa habari na uamuzi wa kutoa mafunzo hayo ni ishara tosha ya ushirikishaji wa waandishi katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa habari sahihi kutoka BoT.


“Tumekutana hapa wakati serikali imepitisha sheria mbili, moja ni ile inayohusu huduma za vyombo vya habari, na ya pili ni ile ya haki ya waandishi kupata taarifa kutoka taasisi za serikali na mimi nikiwa kama msimamizi mkuu katika eneo hili la utoaji habari kwenye taasisi za umma, ninawaalika mtusumbue sana katika kupata taarifa maana utoaji wa habari kwa sasa si suala la utashi tena bali ni  la kisheria.” Alisema Dkt. Abbassi.

Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati akiwasilisha mada juu ya Sheria mpya ya Huduma za vyombo vya Habari wakati wa kufunga semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha mjini Zanzibar

Kaimu Meneja wa Uendeshaji wa Bot, tawi la Zanzibar, Bi.Graceana Bemeye, (aliyesimama), akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Bi. Vicky Msina
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, (Kushoto), akipeana mikono na Mmiliki wa
K-VIS Blog, Bw. Khalfan Said mwishoni mwa semina hiyo

Source: K-VIS Blog/Khalfani Said

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search