KIUNGO WA KIMATAIFA WA YANGA APATA MAJERUHI KATIKA KIPUTE CHA YANGA NA AZAM FC.

Kiungo wa kimataifa wa Yanga kutokea Zambia Justine Zulu jana April 1 2017 ameongezeka katika list ya wachezaji majeruhi wa Yanga ambao watakosekana uwanjani, Zulu ameongeza idadi ya majeruhi baada ya kuumia dakika ya 58 wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC.

Zulu ambaye Tanzania kajizolea umaarufu kwa jina la mkata umeme alichezewa faulo na nahodha msaidizi wa Azam FC Himid Mao na kushindwa kuendelea na mchezo huo na kutolewa nje na nafasi yake ikachukuliwa na Emanuel Martin.

Taarifa za Zulu kutolewa na nje ya uwanja na kushonwa nyuzi 9 mguuni kwake kutokana na nyama zake za ugoko kuchimbika, anaungana kukaa nje ya uwanja na wachezaji wenzake Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko wanaouguza majeruhi, katika game hiyo Yanga ilipata ushindi wa goli 1-0.
No comments:
Post a Comment