#LONDON DERBY YAMALIZIKA KWA SARE ! NI MECHI YA 52 MAN U NA MAN CITY KUKUTANA !

Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 imeendelea usiku wa imeendelea usiku wa jana  April 27 kwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu England kuchezwa katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Mchezo wa EPL leo ulikuwa unazikutanisha timu mahasimu kutoka jiji la Manchester kati ya Man United waliyowafuata Man City katika uwanja wao wa Etihad kucheza mchezo wao wa 33 wa Ligi Kuu England.
Mvuto na upinzani wa Manchester Derby umeongezeka kutokana na upinzani wa kocha Jose Mourinho wa Man United na kocha Pep Guardiola wa Man City ambao walitoka nao toka LaLiga mmoja akiwa anaifundisha Barcelona na Mourinho akiifundisha Real Madrid.
Mourinho na Guardiola leo wamelazimisha sare (0-0) ya 7 toka waanze kukutana katika michezo yao 19 Mourinho akiwa ameshinda mara 4 na kupoteza mara 8 lakini Man City leo wanatoka sare yao ya 52 dhidi ya Man United katika mara zao 174 walizowahi kukutana wakiwa wamepoteza mara 72.
credit: millard ayo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search