Picha 14: Ona Maafande wa 'Kike' walivyojichanganya PSPF ndani ya Mlimani City kwa 'Mafunzo Maalum'

MAAFISA wa polisi waliokuwa wakishiriki mafunzo ya
siku tatu ya polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa
Afrika (SARPCO), wamepata fursa ya kuelewa kwa undani huduma zitolewazo na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mada mbalimbali zilizotolewa na Maafisa wa
Mfuko huo katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
Katika mafunzo hayo Maafisa hao walikuwa wakiongozwa
na Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau) ya Jeshi la
Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda, walipata fursa ya kujua
uendeshaji wa Mfuko huo ambao wanachama wake ni pamoja na Watumishi wote wa
Umma, Sekta binafsi, na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi.
Nae Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina
Mtingwa, aliwaambia maafisa hao wa polisi kuwa, pamoja na kutambua na kusajili
wanachama, kukusanya michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama na
kuweka michango katika vitega uchumi mbalimbali; alitaja majukumbu mengine ya Mfuko
kuwa ni pamoja na kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sharia, kutunza
kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao, kufanya
tathmini ya Mfuko pamoja na kuweka mikakati Imara.
Aidha kwa upande wake, Kaimu Meneja Matekelezo wa
PSPF, Bi.Ritha Ngalo, alizungumzia mwongozo wa ujumuishaji wa michango
(totalization and period of contribution guidelines 2013) kama ulivyofanyiwa
marekebisho kwa polisi waliochangia GEPF na PSPF.
Fuatilia Picha za Matukio mbali mbali wakati mafunzo
hayo maalum yalipokuwa yakiendelea – kwa hisani kubwa ya Khalfan Said wa Kv
blog.
No comments:
Post a Comment