MALIMWENGU: MBUZI KUTUMIKA KULIPIA ADA YA SHULE !
Hali ya kiuchumi nchini Zimbabwe imepelekea Serikali kuruhusu wazazi kutumia mbuzi (mnyama) katika kulipia ada za shule.
Wazazi nchini Zimbabwe
ambao hawawezi kugharimia karo ya shule wanaweza kupeleka mifugo wao kama mbuzi
na kondoo kama malipo, waziri mmoja amesema.
Waziri wa elimu nchini
Lazarus Dokora aliiambia gazeti la Sunday Mail kuwa itabidi shule zilegeze
masharti yao ya kudai karo ya shule kutoka kwa wazazi, na pia kando na mifugo
wanaweza kubali kupewa huduma na ujuzi kama malipo.
"Ikiwa kuna mwashi au
mjenzi katika jamii, yeye yuapaswa kupewa ile nafasi ya kufanya kazi kama njia
ya kulipa karo," gazeti lilimnukuu.
Kuna shule ambazo tayari
zinakubali mifugo kama malipo, Sunday Mail linasema.
Hata hivyo afisa katika
wizara hiyo alifafanua kwamba wazazi ambao wanaweza kulipia watoto wao karo kwa
mifugo ni wale wa mashambani, lakini wazazi walioko mijini wanaweza kulipa
kutumia njia nyingine kama vile kuifanyia shule kazi fulani.
Tangazo hilo lilitolewa
baada ya Zimbabwe wiki jana kupendekeza watu waruhusiwe kutumia mifugo yao kama
mbuzi, ng'ombe na kondoo kama rehani wanapochukua mikopo katika benki.
Katika sheria mpya
iliyopelekwa bungeni wiki hii, wanaohitaji kuchukua mkopo wanaruhusiwa
kuandikisha mali inazohamishika ikiwemo magari na mashine kama dhamana, ripoti
ya BBC World Business ilisema.
Mitandao ya kijamii
ilichukulia habari ya "mbuzi-kwa-karo" na kejeli na ucheshi.
Mwandishi Zimbabwe Tsitsi
Dangarembga aliuliza katika mtandao wa kijamii, Twitter, "kama tungeambiwa
mwaka wa 1970 kuwa tunapigania kutumiwa kwa ng'ombe na mbuzi kama pesa,
tungekubali kupigania uhuru?"
Mmoja wa watumizi wa
mtandao wa kijamii Twitter alisema - Ikizingatiwa kuwa sio wanyama wote
waliozaliwa sawa - je "naweza pata kazi kama mkaguzi wa mbuzi?"
JJMSACKY
No comments:
Post a Comment