Mourinho amtolea macho Dembele


London, England. Jose Mourinho anataka kuichokoza Borussia Dortmund kwa kutangaza nia ya kumataka chipukizi wao Ousmane Dembele.
Manchester United watalazimika kulipa pauni 50milioni ili kuinasa saini ya mshambuliaji huyo Mfaransa.
Dembele (19), alikataa kujiunga na Man United, Chelsea, Arsenal na klabu nyingine kubwa Ulaya na kujiunga na miamba ya Ujerumani akitokea Rennes mwaka jana.
Dembele anaamini kuna nafasi kubwa ya kucheza akiwa Dortmund, kwa sababu ya sera ya klabu hiyo ya kutoa nafasi kwa vijana kucheza kikosi cha kwanza.
Mfaransa huyo alithibisha ubora wake baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ambao Dortmund ilifungwa 3-2 na Monaco.
mcl online

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search