PART 2: NJIA 25 ZA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE
katika sehemu yetu ya kwanza ya jarida letu maridhawa tuliishia mbinu ya kumi ya kupunguza mafuta kwa wanawake.. fuatana na mtabibu wetu katika sehemu yetu ya pili na ya mwisho.
11. KITUNGUU SWAUMU
Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo
(chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili
asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali.
Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka
zaidi.
12. TIKITI MAJI
Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo
lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo
ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.
13. MAHARAGE
Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika
tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia
tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo.
Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa
kuzalisha mafuta mengi tumboni.
Basi kula maharage kila siku.
14. TANGO
Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni
nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango
moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.
15. PARACHICHI
Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma
mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba).
Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni
mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma
mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.
Kula parachichi 1 kila siku.
16. TUFAA
Kula tufaa maarufu sana kama 'apple' (epo) kunaweza kusaidia
kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta
kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi
sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.
Hivyo kula tunda hili 1 kila siku asubuhi kupunguza shauku
yako ya kutaka kula zaidi ndani ya hiyo siku nzima.
17. MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni mbadala mzuri kabisa katika kuchoma
mafuta ya tumboni. Mafuta ya samaki yenyewe hulenga kuyachoma moja kwa moja
mafuta yanayozidi tumboni. Ukiweza unaweza kuamua yawe ndiyo mafuta yako ya
kupikia, pia unaweza kunywa mafuta haya kijiko kikubwa kimoja kila siku
unapoenda kulala.
18. SIAGI YA KARANGA
Siagi ya karanga hupunguza njaa na kuongeza nguvu katika
mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho
kama 'niacin' ambacho chenyewe huzuia mafuta kujilundika tumboni. Hivyo kwenye
mkate wako asubuhi ningekushauri utumie hii siagi ya karanga badala ya mafuta
mengine ambayo si salama, pia unaweza kutumia hii siagi ya karanga kama mafuta
yako ya kuunga katika mboga nyingi unazopika hata katika wali unaweza kutumia
kama mafuta yako mbadala.
19. MAYAI
Mayai yana vitamini nyingi sana ndani yake (mayai ya
kienyeji lakini) na yana madini pia kama kalsiamu, zinki, chuma, omega -3 nk.
Viinilishe vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni.
Hivyo kula mayai asubuhi kila siku ili kuondoa na kupunguza mafuta mwilini.
Mayai pia ni moja ya vyakula vinavyomfanya mtu ajisikie kushiba kwa muda mrefu
bila kuhitaji kula kula tena.
20. CHAI YA KIJANI
Chai ya kijani maarufu kama 'Green tea' hufanya kazi ya
kuondoa sumu mwilini jambo linalosaidia pia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini.
Kunywa chai hii ya kijani kila siku kutafanya ngozi yako kukua vivyo hivyo
kufanya tumbo lako kukaa sawa bila kuwa na mafuta mengi.
21. MTINDI
Ingawa mtindi unaweza kupelekea kuongeza uzito zaidi, hata
hivyo mtindi mtupu kabisa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake
unaweza kukusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku yasizidi
kikombe kimoja (robo lita). Pia mtindi ni moja ya vyakula vinavyoweza kukufanya
ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea njaa ya kutaka kula.
22. JUISI YA KOTIMIRI
Juisi ya kotimiri (Parsley juice) huondoa sumu na takataka
nyingine zozote mwilini, pia huchoma mafuta na nishati. Kotimiri ni dawa nzuri
kwa matatizo mbalimbali ya figo pia kwa kuchoma mafuta mwilini.
Pata kikombe kimoja cha juisi hii kila siku unapoenda
kulala.
23. NDIZI
Kama lilivyo tufaa, ndizi pia zina kiasi kingi cha potasiamu
na vitamini za aina mbalimbali ndani yake. Ukipenda kula ndizi kila mara
zinachofanya mwilini mwako ni kuondoa ile hamu ya kutaka kula vyakula feki
(fast food). Zaidi sana ndizi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
na hivyo kupelekea mafuta ya tumboni kuyeyuka kirahisi zaidi. Kula ndizi kila
siku ukiweza ukiamka tu kula ndizi zilizoiva 3 mpaka 5 kila siku.
24. MAJI YA KUNYWA
Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia pia kupunguza
uzito. Kunywa maji lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu. Kunywa maji
kidogo kidogo kutwa nzima. Hili halitafanya kazi ya kusafisha mwili tu bali pia
litafanya ngozi yako kung'aa na kukuwa. Nywele zako pia zitaonekana ni zenye
afya na mwili mzima utakuwa ni wenye kuvutia.
Kitu cha kwanza ukiamka tu ni kunywa maji glasi 2 na
uendelee hivyo hivyo glasi moja moja kila baada ya lisaa limoja au mawili kutwa
nzima. Maji ni uhai, bila kunywa maji kila siku ni sawa na kwenda dukani bila
hela mfukoni.
Asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako
ni maji, asilimia 27 ya mifupa yako ni maji, asilimia 75 ya mwili wako ni maji.
Sehemu kubwa ya dunia hii imefunikwa na maji na sehemu yenye ardhi ni kipande
kidogo sana. Haijalishi unaishi kwenye baridi au kwenye joto hakikisha
unakunywa maji ya kutosha kila siku, huhitaji kusikia kiu au hamu ndipo unywe
maji, hapana maji ni lazima uyanywe tu hata iweje.
25. MAZOEZI YA KUTEMBEA
Shida kubwa kwa kina mama wengi wa kiTanzania ni kuwa
hawajishughulishi na mazoezi. Hapa Tanzania mazoezi inaonekana ni jambo la
wanaume tu. Mazoezi ni jambo la lazima kwa mtu yeyote iwe unaumwa au huumwi.
Ili kuchoma mafuta mwilini kwa haraka zaidi tembea kwa miguu
mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku. Kumbuka nimesema lisaa limoja yaani
dakika 60 bila kupumzika (none stop) kila siku. Kutembea kwa miguu lisaa limoja
huamsha mwilini kimeng'enya kijulikanacho kama 'lipase' ambacho chenyewe huamka
tu ikiwa utatembea bila kusimama kwa dakika 60 na kikishaamshwa (when it is
activated) huendelea kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12 mfulululizo.
Usiseme nikitoka sehemu fulani kwenda sehemu fulani nitakuwa
nimetembea vya kutosha, hapana, unahitaji uwe na saa mkononi kuhakikisha kweli
dakika 60 zimeisha ukiendelea kutembea bila kusimama. Kama utaweza kukimbia
kidogo kidogo (jogging) basi utachoma mafuta ya tumbo kwa haraka zaidi.
Ufanye zoezi hili kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili
mfululizo na mafuta kwenye tumbo lako yatapotea yenyewe bila kupenda.
Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.



No comments:
Post a Comment