Waziri Mwigulu apokea tani 360 za cement...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu,Tanga
WAZIRI wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba amepokea tani 230 za cement kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi Pemba na tani 130 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali na mabweni ya wanafunzi katika Jimbo la Iramba kutoka kiwanda cha Simba cement mkoani Tanga.
Waziri Mwigulu akipokea mifuko ya cement kutoka kiwanda cha Simba Cement mkoani Tanga
Waziri Nchemba amekishukuru kiwanda cha simba kwa kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii hasa kusaidia serikali katika ujenzi wa nyumba bora za askari polisi na ujenzi wa hospitali na mabweni.
Dk. Mwigulu ameyasema hayo leo mkoani Tanga katika kiwanda cha simba cement na kuwataka watanzania na wafanyabiashara wenye uwezo kuchangia shughuli za maendeleo nchini kama kujenga vituo vya polisi, nyumba za askari polisi,magereza na zimamoto ili kuwapa morali ya kazi zaidi vijana wanaofanyakazi saa 24 kulinda raia na mali zao.
"Mimi kama Waziri nawashukuru Simba cement kwa kuisaidia wizara yetu zaidi ya mifuko 5500 kwa ajili ya kusaidia polisi pemba ujenzi wa nyumba za askari ambao wanaishi katika mazingira magumu, rai yangu kwa watu wenye uwezo tunawakaribisha," amesema Dk Mwigulu.
Mwenyekiti wa Halamsauri ya wilaya ya Iramba, Saimon Mkumbo Tyosela amemshukuru Dk Mwigulu kusaidia kufanikisha kupatikana kwa cement ambazo zitatumika kwenye ujenzi ambao ulisimama kutokana na kukosekana kwa fedha za kuendeleza ujenzi huo na kusema sasa tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike katika wilaya ya iramba linakwenda kupungua kama si kuisha kabisa.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Simba cement, mhandisi Reinhardt Swart amesema wanasaidia shule zilizo katika Mkoa wa Tanga lakini sasa wameamaua kusaidia taasisi zingine za serikali zinyeuhitaji wa kuboresha miundombinu kama wanavyofanya kwa polisi Pemba na shule na hospitali za Iramba.
Waziri Mwigulu alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha Simba cement kuangali namna wanavyochimba malighafi hadi uzalishaji wa cement unavyofanyika kiwandani hapo ambacho kimeajili watanzania 300 na vibarua 3000.

No comments:
Post a Comment