#TANAPA YAFAFANUA MAJERUHI WA SIMBA ! NI MLINZI WA KAMPUNI HIFADHI YA TARANGIRE !
Idara ya mawasiliano Hifadhi za Taifa Tanzania imetoa taarifa rasmi kuondosha mkanganyiko na uvumi ulioenea juu ya aliejeruhiwa katika tukio la kuvamiwa na simba kwa mlinzi wa kampuni binafsi ya ulizi inayofanyia shughuli zake katika hifadhi ya Tarangire na si vyenginevyo.
Majeruhi anaendelea na matibabu na TANAPA imewakumbusha watumiaji wa mitandao kuzingatia weledi na miiko stahiki katika kusambaza taarifa na picha ambazo hazijathibitishwa,
TANAPA imewahakikishia usalama wageni wote watembelea hifadhi za Taifa.
...mwisho..
No comments:
Post a Comment