TFDA yapokea maombi ya viwanda 767


Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TDFA), Hiiti Sillo amesema kuanzia Machi mwaka huu taasisi yake ilimepokea maombi mapya ya usajili wa viwanda 767.
Amesema katika maombi hayo, viwanda 635 vipya vimesajiliwa kati ya hivyo, 613 vya chakula, kimoja cha dawa na 21 vya vipodozi akisema hiyo ni asilimia 82.8 ya maombi yote jambo linaloashiria kwamba waombaji wengi wanazingatia sheria.
Amesema katika kipindi hicho TFDA ilifanya tathmini ya maombi 4,762 sawa na asilimia 82.1 ya usajili wa bidhaa za dawa, chakula, vifaatiba na vipodozi, kati ya maombi 5,802 yaliyowasilishwa na 4,322 (75%) yaliidhinishwa na 440 yalikataliwa kwa kutokidhi vigezo vya ubora.
Sillo ameeleza hayo leo kwenye mkutano na wahariri wa vyombo vya habari walipokutana mkoani Tabora.
Source: Mwananchi mobile

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search