TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MOYO KWA MTOTO ALIYEPO TUMBONI KWA MAMA YAKE (FETAL ECHO)

MUH1

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo upimaji wa kina mama wajawazito  moyo wa mtoto aliyepo tumboni (Fetal ECHO) ili kuangalia kama una magonjwa au la. Kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kufahamu afya ya mtoto aliyepo tumboni ikiwa ni pamoja na hali ya moyo.

MUH2MUH3
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimpima Mama Mjamzito  moyo wa mtoto aliyepo tumboni ili kuangalia kama una magonjwa au la. Mwishoni kwa mwaka jana Taasisi hiyo iliwapima wajawazito  25 kati ya hao watano watoto wao walikutwa na matatizo ya Moyo.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
source: habari za jamii

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search