Timu nne zilizofanikiwa kuingia nusu fainali ya UEFA Champions League


Usiku wa April 19 2017 michezo ya pili ya robo fainali ya UEFA Champions League ilichezwa barani Ulaya, FC Barcelona waliwakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia wakati AS Monaco walikuwa wenyeji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani katika michezo hiyo ya marudiano.
Barcelona ambao walikuwa wanahitaji ushindi wa kuanzia goli 4-0 ili wasonge mbele dhidi ya Juventus kutokana na mchezo wa kwanza kufungwa kwa magoli 3-0, wamejikuta wakiaga mashindano kwa kulazimishwa sare tasa ya 0-0, huku Dortmund wao wakiomdolewa katika hatua hii kwa ggregate ya 6-3.
Dortmund wao mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani walipoteza kwa kukubali kufungwa magoli 3-2, hivyo mchezo wa marudiano walipaswa kupata ushindi walau wa magoli 2-0 ili wasonge mbele, bahati haikuwa kwao na wamejikuta wakiambulia kipigo cha magoli 3-1, ratiba ya nani atacheza na nani itajulikana ijumaa hii.

Source: Ayo Tv

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search