VIDEO: LEMA AWAONYA WANAOTAKA KUMTEKA; ASEMA 'WATASUBIRI SANA'

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya watu aliodai kuwa wamemuweka kwenye orodha ya wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Dodoma, Lema amedai kuwa yeye haogopi vitisho vya kutekwa na kwamba wanaopanga kumteka wanapaswa kufahamu kuwa hawatafanikiwa na kwamba hakuna atakayeweza kusababisha kifo chake isipokuwa Mungu pekee.
“Ninawaonya watekaji, kwamba ninamjua Mungu ninaemwamini, kwamba hawataliona kaburi langu wala mauti yangu kwa sababu Mungu ninayemuamini najua nguvu zake na najua uwezo wake,” alisema Lema.
“Kwahiyo mimi kutekwa haitawezekana, kuuawa na mtu haitawezekana kwa sababu namtumaini Mungu kwa nguvu zangu zote,” aliongeza Mbunge huyo.
Kauli hiyo ya Lema imekuja kufuatia kauli ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeeleza jana Bungeni kuwa alionywa na baadhi wa watu wakiwemo mawaziri kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge kumi na moja walio kwenye mpango wa kutekwa na genge la watu wasiojulikana.
Msikilize hapa kwa undani:(Source: Dar24.com)



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search