VIDEO: 'ROMA MKATOLIKI' AMNYANYUA MBUNGE KESSY BUNGENI.. ASEMA AMESIKITISHWA SANA NA MANENO YALIYOMO KWENYE WIMBO WAKE !!

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy amedai kuwa msanii Roma Mkatoliki amerekodi wimbo ambao una lugha ya matusi dhidi ya Rais, na kulaani kitendo hicho.
Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma, Kessy ambaye alionesha kuumizwa na kitendo cha kuandika na kurekodi nyimbo zenye lugha za kuudhi dhidi ya Mkuu wa nchi alihoji uhuru na demokrasia inayotoa nafasi hiyo.
“Wewe unamtukana Rais wa nchi umekuwa nani? Uhuru gani, demokrasia gani hii. Unaimba wimbo na mtu wa studio anarekodi, ama kweli huu sio utawala… wangeniachia mimi dakika mbili niwaoneshe hawa,” amesikika Kessy.
“Haiwezekani, Mkuu wa nchi anatukanwa. Ukiusikia huo wimbo wa Roma sijui Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu. Haiwezekani mtu anaachia wimbo kama ule halafu unamshabikia tu,” aliongeza.
Kessy alidai vitendo kama hivyo haviwezi kuonekana katika nchi za jirani pamoja na nchi za Uarabuni huku akitaja hatua kali ambazo zingeweza kuchukuliwa katika nchi hizo.
Angalia video kwa habari zaidi:(SOURCE DAR24.COM)



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search